WAPATA WACHUMBA:
Kwa heshima na taadhima nadiriki kuja mbele ya blog hii kutoa AHSANTE kwa baadhi ya wanachama/watumiaji wa blog hii kwa jinsi ambavyo wamekuwa wazi na ku-share stories zao kuhusu jinsi blog hii ilivyowasaidia kuwaunganisha na watanzania wengine duniani kote.
Ni jambo la kujivunia na kutia moyo kuona jinsi watu wanavyoitumia blog hii katika kufanikisha ndoto zao za kukutana na marafiki au wachumba ulimwenguni kote.
Hadi sasa wamefika member 16 kuomba kuondoa profile zao hapa baada ya kuonana na wenza. Hata hivyo kwa wote amabo mmekutana na muwapendao, nakuombeni mzidi ku-share stories zenu kwa wengine ambao hawajawahi kusikia wabongomeet au kama wamesikia lakini hawajatumia ili waweze kutumia. Vilevile mnazidi kukaribishwa kwa maoni tofauti ambayo yatasaidia kuendeleza na kuboresha hii huduma.
NAKUTAKIA DATING NJEMA.
Da Jose.