Watanzania wenzangu pamoja na wapenzi wa blog hii. Napenda kuwajulisha kuwa nimefungua akaunti na facebook. Najua watu wengi waliniomba hilo na sasa nimewasikiliza. Hivyo naamini twaweza kuunganisha nguvu pamoja ili kuwakutanisha watu wengi zaidi.
Ila naomba niwe wazi, sikufungua facebook au blog hii kutafuta mchumba maana tayari kuna watu tayari walianza longolongo za kuimba kwaya kwenye email. Mimi nina mme na mtoto. Lengo la kufungua hizi social media ni kupenda kuwakutanisha watu kutoka pande zote za dunia. Kama ambavyo niliongelea kwenye profile yangu hapa kuwa mimi nilikutana na mme wangu kupitia social media kama hivi,
Kama mimi nilifanikiwa, kwa nini wewe husifanikiwe.
Wale ambao watashindwa kutumia vizuri blog hii nitawa-block (Blog na facebook). Sitanii kwa hili maana napenda ku-set standard kwa hizi sites, ukishindwa kujiheshimu utakutana na ban.