Karibuni kwenye Wabongomeet Blog

Jitafutie rafiki na mchumba hapa Wabongomeet.....


Kwa wale wote ambao watapenda kuweka picha pamoja na info zao, tafadhali tuma kwa kupitia email wabongomeetinfo@gmail.com Nakaribisha maswali pamoja na maoni yenu.







Saturday, September 10, 2011

Mtiririko wa kutengeneza PROFILE hapa.

Ndugu zangu ufuatao utakuwa mtiririko wa kutengeneza profile ya kujitafutia aidha mchumba au rafiki. Hii ni format itakayokubalika hapa, hivyo nakushaurini mfuate huo mtiririko kama ulivyo hapa chini:

Jina langu: Weka Jina lako
Jinsia yangu: Taja jinsi yako
Umri wangu: Taja umri ulionao
Natafuta: Taja jinsia unayotafuta
Umri wake: Taja umri wa mtu umtafutaye.
Kwa uhusiano kama: Taja uhusiano unaohitaji kuwa na huyo mtu umtafutaye.
Nchi unayoishi: Taja nchi uishiyo hata kama ni nje ya Bongo
Umbo langu: Jisikie huru kutaja umbo lako (Mnene, mwembamba kiasi au vyovyote)
Kazi yangu: Kazi unayofanya
Muonekano wangu: Mrembo au ujionavyo wewe.
Mshahara: Siri yangu (Unaweza kutaja kama hujali)
Oa/Olewa: Sijaolewa/ Nimeoa/ Nimetariki(divorced)
Mtoto: Nina mtoto 1/ au naishi na watoto 3 (Unaweza kuwa na mtoto mmoja wa kuzaa lakini unaishi na watoto wa wengine)
Dini yangu: Taja dini yako mwenyewe.
Dini yake: Taja dini ya mtu umtafutaye
Sigara (mimi): Taja kama unavuta (Sivuti/ Navuta)
Sigara (yeye): Taja kama unahitaji mvutaji (Mvutaji/ Si mvutaji)
Pombe (mimi): Taja tabia yako ya unywaji (nakunywa kiasi/ Mlevi nk)
Pombe (yeye): Taja tabia ya unywaji kwa umtafutaye.
Email: Weka anuani ya email yako.
Simu: Unaweza kuweka namba kama hujali au vyoyote unavyoona wewe.
Maelezo Zaidi:
Hapa jaribu kujieleza aidha kwa kirefu au kifupi ili mradi mtu aweze kupata picha mawazoni kuwa wewe ni mtu wa namna gani. Hapa unaweza kutaja hobbies na interests.
Kama una swali tafadhali husisite kuniandikia, nitakujibu mapema iwezekanavyo.

1 comment: